Bintiye askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana Afrika kusini, Desmond
Tutu, ameshurutishwa kuacha kazi yake ya ukasisi wa kanisa la kianglikana baada
ya kufunga ndoa na mwanamke kinyume na sheria za kanisa hilo.
Mpho Tutu-van Furth
sasa amevuliwa madaraka ya kuongoza ibada zote za kidini kwani kanisa hilo
linapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja.Kanisa la kianglikana nchini Afrika
kusini linapinga vikali ndoa za wapenzi wa jinsia moja, japo ndoa hizo
zilihalalishwa nchini humo miaka 10 ilopita.
Bintiye Tutu(Kushoto)akiwa na mkewe |
Baada ya binti wa
aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini humo desmond Tutu, kumwoa
mwanamke mwenzake, ilibidi avuliwe majukumu yake kama kasisi.Kwa sasa Mpho
Tutu-van Furth hatohusika na majukumu yake ya hapo awali ya kidini yakiwemo,
kuongoza ibada za mazishi, kuongoza sakramenti takatifu na pia hataongoza
sherehe za harusi.
Babake mzazi , Askofu
mstaafu Desmond tutu alihuzunishwa sana na taarifa hiyo, japo hakushtuka saana.Bi
tutu anakiri wazi kuwa sheria za kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini
zinaelezea wazi kuwa ndoa ni kati ya mwanamke na mwanamme.
Askofu Desmond Tutu na bintiye |
Anasema baada ya
kufunga ndoa, askofu wa kanisa la Saldanha Bay alishauriwa kufuta leseni yake,
lakini Bi tutu aliamua kuirejesha yeye mwenyewe kabla ya kunyang'anywa.Wachumba
hao wapya, Mpho na Marceline Tutu-van Furth wamekuwa fungate katika kisiwa cha
Indonesia cha Bali.Kila mmoja ana watoto, kutoka kwa ndoa ya awali.
Desmond tutu ambaye
kwa sasa ana umri wa miaka 84, afya yake imedhoofika, lakini hilo halikumfungia
kuhudhuria harusi ya bintiye mapema mwezi huu.Bwana tutu amewahi kuskika
akiunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
0 comments:
Post a Comment