Ripoti za vyombo vya habari vya Israel
zinasema polisi wamependekeza kufunguliwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya mke wa
waziri mkuu wa isral, Benjamin Netanyahu kwa shutuma za matumizi mabaya ya
fedha za umma kwa makazi rasmi na binafsi.
Sara Netanyahu ambaye anakanusha kufanya
makosa yoyote alihojiwa na polisi mwaka jana kuhusiana na uchunguzi wa fedha za
umma alizolipwa mhudumu aliyekuwa anamuangalia baba yake kabla ya kifo cha baba
huyo.
Uchunguzi ulichochea ukaguzi wa mahesabu
ya serikali pia ulilenga kwenye fedha zilizotumika kwa matengenezo ya umeme
kwenye nyumba binafsi ya Netanyahu katika eneo la mapumziko la pwani huko
Caesarea.
Hakukuwa na ishara yeyote siku ya
Jumapili kama waendesha mashtaka watakubali mapendekezo ya polisi.
Msemaji wa waziri mkuu siku ya Jumapili
alikanusha kabisa kufanyika kwa kosa lolote. “Haya ni masuala ambayo hata
hayakaribii uvunjifu wa sharia”, alisema Nir Hefez katika taarifa yake. “Tuna
uhakika kwamba wakati mamlaka itakapoangalia ukweli halili watagundua kwamba
hakuna jambo lolote”, alisema.
Ripoti zinasema uchunguzi huo pia
ulichochewa na ushahidi kutoka mlinzi wa zamani katika makazi rasmi ya
Netanyahu.
Mapema mwaka huu mlinzi huyo alishinda
kesi ya kuumizwa kihisia baada ya mahakama ya kazi kutoa uamuzi kwamba Sara
Netanyahu mara kwa mara alimtendea vibaya mkuu huyo na wafanyakazi wengine wa
nyumbani.
Moja ya ugunduzi wa mahakama ambao
uliungwa mkono na ushahidi ni kwamba Sara Netanyahu wakati mmoja alitupa chini
chombo cha kuwekea maua ambapo maua hayo yalikuwa na siku moja tu wakati
akimkaripia mfanyakazi huyo na kumueleza kuwa maua hayo si mazuri ya kutosha.
0 comments:
Post a Comment