NDOA:Taasisi Ya Utumwa Wa Hiyari Inayoelekea Kupoteza Mvuto Wake


 

Na:Bonaventure

“Una matatizo ya kiafya…”, “wewe ni mbinafsi”, “utaishia pabaya” n.k, haya ni baadhi ya maneno na tabiri ambazo wamekua wakizipokea watu woote ambao wameshadhihirisha kwenye jamii kua wao kamwe hawata oa wala kuolewa..kichwa cha Makala hii kinaeleza mambo kadhaa kuhusu mwandishi..
i)                    Kama mwandishi..natambua na kuamini kua ndoa ni taasisi.,
ii)                  ii) Kama mwandishi natambua kua Ndoa kwa wakati na miaka Fulani..ilikua ni taasisi yenye mvuto na heshma kwenye jamii..
Ni wajibu wa Makala hii kukuonesha kwanini ndoa sio taasisi yenye mvuto tena na miaka michache kutoka sasa..litakua ni jambo la kustaajabisha kusikia fulani anaoa au anaolewa..
Ndoa ni nini? Ifahamike kwamba ndoa inayoongelewa hapa ni ndoa baina ya mwanaume na mwanamke na si vinginevyo..ndoa inafahamika kua ni muunganiko rasmi kati ya mtu mume na mtu mke kwa lengo kuu la kuishi pamoja..ikiwa ni pamoja na kushirikishana mali,hisia,mwili na matatizo J.katika tafiti hii niliyofanya muda mrefu..niliamua kuongea na wanandoa 25..swali kubwa lilikua Kwanini umeoa/umeolewa?, yafuatayo ni majibu mbalimbali ambayo yalijirudia.
-Nimeoa/nimeolewa kwa sababu ndio utaratibu..sasa utaishije mwenyewe.
-Nimeoa/nimeolewa kwa sababu ya familia.kuzaa na kulea watoto na kupata waridhi nikifariki.
-Nimeoa/nimeolewa kuongeza heshma yangu kweye jamii
-Nimeoa/nimeolewa kwa sababu ni muhimu..nikizeeka nani atanihudumia
-Nimeoa/nimeolewa kuboresa mausiano yangu..na kumfanya mwenzangu aniamini,kuthibitisha kua nampenda.
-Nimeoa/nimeolewa ili kuepuka kuwa na wapenzi wengi.
-Sijui kwanini nilioa/niliolewa..niliona ni kawaida tu.
-Nilioa/niliolewa kwa sababu nilipata ujauzito (mwanamke).
-Nimeoa/kuolewa kwa sababu dini yangu inanitaka nifanye hivyo.
 
Hizo ndio sababu ambazo zimekua zikijirudia..kama sababu yako haipo kwenye mtiririko huo..nitafurahi ukiniambia nijifunze Zaidi, Ndio…wako waliosema kweli kua hawajui kwanini waliingia kwenye taasisi hii.swali la msingi..Je? ni sababu gani kati ya hizo inaweza kukufanya kweli utamani ndoa? Ni sababu gani kati ya hizi inaweza kukufanya ukubali kubeba mzigo huu na jukumu la kustawisha ndoa?
 
Asilimia 90 ya sababu zote zilizotajwa ..zinaweza kuwekwa kwenye kapu moja..MAPOKEO,tuko karne ya 21, tuko kwenye mwaka 2016..ni vema ukajipa changamoto..je ? unafanya mambo kwa mazoea? Kwa sababu ni kawaida? Neno kawaida limekua zito na linaheshimika miaka hii..popote ambapo mtu atafanya jambo..halafu kama mtazamaji tu ukaamua kumuuliza..ni kwanini umefanya jambo hili,kujibiwa “kawaida” ni kawaida. Kama upo tayari ..basi endelea kuungana na mimi tuone kama kweli kuna sababu yoyote nzito iliyobaki inayoleta hamasa ya kua kwenye ndoa.
 
Tuchimbe neno  “kawaida”
 i/kuoa kwa sababu ya familia/watoto na waridhi wa mali nikifariki: je? Ni kweli kwamba bila ndoa hivi vyote haviwezi kupatikana? Hapana..sio kweli, ni dhahiri kuna ndugu zetu wengi wanaohangaika kutafuta pahala pa kuishi,Tanzania kwa sasa ni moja kati ya mataifa yaliyo na wimbi kubwa la watoto wasio na walezi (watoto wa mitaani)..kuna chaguo la kuasili (Adoption)..kumlea mtoto uliyemu asili tangu akiwa kichanga..haina tofauti na kumlea mtoto alipatikana kwenye ndoa, usumbufu unaweza kutokea ndio..ila hata waliozaa wanasumbuliwa na watoto wao pia.kuoa ili kuzaa ili kupata mridhi wa mali..ni sababu kuntu? Hata kidogo, una haja gani ya mali zako baada ya kifo?
 Kila ulichonacho..mali na pesa zote ..vipo kwa ajili ya kukurahisishia maisha pindi ukiwapo hapa duniani.ukifariki..huna haja navyo..hivyo basi..hii sio sababu nzito.
Hitimisho: sababu hii imetawaliwa na ubinafsi, Je mwanandoa alienipa hii sababu na yule ambae ameamua kubaki mwenyewe (bila ndoa) nani ni mbinafsi Zaidi ya mwingine?
 
Ii/ kuongeza heshma kwenye jamii: je? Ni kweli,miaka na miaka imepita tunashuhudia watu wengi mashuhuri ambao hawakupata kua kwenye ndoa wakiwa wanaheshimika hadi leo..wako wanasiasa..wako wanasayansi..wako vijana n.k, ndoa sio kigezo pekee cha kuleta heshma kwenye jamii..wako wanandoa wengi waliopoteza heshma zao baada ya kujidhalilisha kwenye jamii..ilihali walikua kwenye ndoa bado walipoteza heshma
 
Iii/ Nikizeeka nitakua na mtu wa kunihudumia: katika kuangalia ili suala ni vema tuwe wadadisi kidogo..wako wanaume wengi wanaoachwa miaka hii baada ya kupata matatizo..nitaeleza mfano mdogo halisi..nimepokea barua pepe kutoka kwa kijana rafiki (jina linahifadhiwa) ambae ni raia wa marekani ”
“habari .,naomba kukueleza kwa ufupi juu ya marehemu baba yangu..labda itakusaidia endapo utakua na mpango wa kuoa kwa woga wa kubaki mwenyewe/(die alone),usifanye hivyo..katika dakika za mwisho za uhai wa baba yangu ambae alikua anaugua kansa…niliona ni kwa jinsi gani mama yangu alivyoonesha kutokujali..aliona ugonjwa wa baba yangu ni usumbufu kwake na hata alimlaumu kwa kuugua kansa kwamba ni sababu ya kuvuta kwake sigara..miaka ya mwanzoni 1970 huku akisahau kabisa ni miaka hiyo hiyo ambayo baba yangu aliacha kabisa kuvuta sigara,sitasahau pale ambapo mama alipinga baba kurudishwa nyumbani ..augulie akiwa nyumbani kwa kigezo kikubwa kua asingeweza kumuangalia.., mama pia hakuajiri nesi wa kumuangalia..aliongea maneno hayo mbele ya baba na daktari..baba ambae kwa kipindi hiki hakua na uwezo wa kuongea tena..badala yake akampeleka kwenye vituo vya malezi (rehab cetres) …..”
 
Barua hii inaendelea na ni ndefu..Je? wewe uliyeoa/kuolewa …una unakika huyo uliyenae atakua pamoja na wewe kipindi chako cha uchungu? Kubaki peke yako kipindi cha uchungu inaweza kua nafuu kuliko kubaki na mtu ambae ulidhani anakujali..ila akawa hana muda na wewe/hakujali.
 Sababu nyingine zilizobaki..zote kwa pamoja zikipitiwa moja baada ya nyingine ni dhahiri hazina uzito wowote, tafiti iliyofanywa kuhusu wadada wanaojiunga mitaa mingi ya jiji (dada poa) ilitanabaisha wazi kua wateja wao wengi ni waume za watu., kutoka nje ya ndoa (infedility) limekua jambo linaloitwa “kawaida” ,limetungiwa hadi jina “kuchepuka” na hakuna lolote linalofanyika….kwa wale wasio na kifua cha kuhimili wizi huu wa mapenzi..huishia kujiua.

(Makala Haya Ni Mawazo Ya Mwandishi Na Wala Sio Msimamo Wa Mtandao Huu)
 

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment