Haiko
wazi sana lakini katika watu Rais Dilma Rouseff hatamsahau basi ni makamu wake
Michel Temer.Makamu huyu wa Rais ambae sasa ndiye anaekalia kiti hicho baada ya
Rais Dilma kusimamishwa kazi hata hapo mashtaka yake yatakapomaliza kusikilizwa
ndani ya siku 182 ndiye hasa alienyuma ya mpango huu.
Temer
mwanasheria nguli na mwanasiasa mkimya ila mahiri mwenye asili ya Lebanon na
mwenyekiti wa chama cha Brazillian Democratic Movement Party (PMDB) ndiye anaetajwa kama The man behind the scene.Makamu huyu wa Rais sasa atakaimu nafasi
ya Rais mpaka hapo suala la Rais Dilma litakapomalizwa na kuonekana hana hatia.
Kwanini Temer amehakikisha anamtoa
Dilma madarakani?
Temer
na Dilma wanatoka vyama tofauti vya siasa kwa hiyo ni wapinzani.Kutokana na
hali hiyo Rais Dilma amekuwa akimtenga Temer kwenye mambo mengi ya shughuli za
serikali hata wakati mwingine kufanya maamuzi pasi kumshirikisha kabisa makamu
wake. Lakini ikumbukwe kama kunatokea tatizo basi ni serikali nzima inakuwa
ikilaumiwa jambo ambalo limekuwa likimkera sana Temer na amekuwa akimlalamikia
sana Rais Dilma juu ya hilo.Hivyo watu hawa wawili wamekuwa wakiishi katika
hali ya kutoelewana.Na ilipotokea sakata la Rais kudaiwa kutumia fedha za
serikali vibaya na kutoa taarifa za uongo juu ya akiba ya serikali ndipo hapo
Temer alipoanza kutumia mwanya huo kutimiza azma yake.
Kutoelewana
kati ya Temer na bosi wake kuliibuka hadharani Desember mwaka jana (2015) pale
alipomwandikia barua bi Dilma akilalamika kutengwa katika shughuli za serikali
na mambo yote kuyafanya Rais mwenyewe.Barua hiyo iliyoanza na maneno ya kilatini
"Verba Volant, Scripta Manent" (Maneno yanayosemwa hupaa,yanayoandikwa hubaki) ilieleza kuwa mawasiliano
hayo ni binafsi kati yake na Rais na kama Rais ataendelea na tabia hiyo ya
kutemtenga katika shughuli za serikali basi matatizo yoyote yatakayompata
asihusike.
Katika barua hiyo alimlalamikia Rais Dilma kuwa amemfanya yeye kama Makamu
wa Rais pambo badala ya kuwa Makamu wa Rais anaefanya kazi.Barua hiyo ilivuja
katika mitandao ya kijamii japo alimsisitiza Rais kuwa iwe baina yao
wawili.Baada ya kuvuja ilichorwa katuni ikimwonyesha Temer kama pambo la
Christmass na Rais Dilma akimcheka kwa dharau.Ofisi ya Rais haikutoa tamko
lolote juu ya hilo na badala yake Rais Dilma alitoka hadharani na kumwita
msaliti katika serikali yake.
Baadae mwezi April mwaka huu rekodi ya sauti ya Temer ilivuja iliyosikika akiwasihi wabunge wa chama chake kuwa
wasitarajie kama kukitokea mabadiliko ya utawala basi mambo mazuri yataanza
kuonekana ndani ya muda mchache.Rekodi hiyo inachukuliwa kama ushahidi kuwa
tayari alishaanda mazingira ya kuongoza kumtoa Dilma kwenye kiti jambo ambalo
leo limetimia na sasa yeye ndio Rais.
Ungependa kujua
hili…..
Temer ana watoto watano.Watatu aliwapata na mke wake wa kwanza, mmoja
alizaa na mwandishi wa habari na mmoja amezaa na mke wake wa sasa ambae alianza
nae mahusiano akiwa na miaka 17 wakati yeye Temer akiwa na miaka 60.Sasa hivi
Temer ana miaka 75.
0 comments:
Post a Comment