Bundi
anazidi kumwandama bi Hilary Clinton katika harakati zake za kuwania kiti cha
urais wa Marekani.Sasa yagundulika kumbe sio kwamba alitumia barua pepe peke
yake kwa mawasiliano ya kiofisi bali hata simu yake ya nyumbani.
Nyaraka
mpya za idara ya serikali inayoshughulikia mambo ya nje zimetolewa jana
Alhamisi na waangalizi wa kujitegemea zinazoonyesha kuwa Hilary aliwahi kuamua
kutotumia simu za ofisi zenye usalama wa kutunza siri anazotakiwa kutumia kwa
jambo lolote la kiofisi badala yake alitumia simu yake ya mkononi aina ya
Blackberry kufanya mazungumzo ya kiofisi kwa madai kuwa mtandao wenye usalama
wa mawasiliano ya kiofisi ulikuwa ukimsumbua.
Nyaraka
zinaonyesha kuwa tarehe 22 February, 2009 Hilary alimwandikia barua pepe
aliyekuwa msaidizi wake mkuu bi Cheryl Mills (Aliehojiwa juzi na FBI na
kutoroka) akimweleza kuwa anajaribu kutumia simu ya ofisi lakini mtandao
unamsumbua hivyo amekata tamaa na anaanza kutumia simu yake ya kiganjani.
Mawasiliano hayo aliyafanya mara tu alipokuwa ametoka safari ya kikazi nje ya
nchi.
Barua
pepe hiyo inanukuliwa ikisema “Nimewapigia wahusika wamenipa hii namba yako
yenye usalama lakini nakupigia inatoa sauti kali sana” Mills akamjibu “Jaribu
tena” Hilary akajibu “” Nimeshaka tamaa.Nipigie wewe kwa simu yangu ya nyumbani”
Kinacholeta
shaka ni je baada ya hapo waliongea nini kwa hiyo simu ya nyumbani?Je
hakuendelea na mtindo huo?.
0 comments:
Post a Comment