Na:Lello
Mmassy
Itakuwaje
leo ukiambiwa tunasitisha matumizi ya mawasiliano kwa njia ya simu,kuwa ili
uwasiliane na ndugu yako alieko kijiji cha Kapalamsenga kule Sumbawanga basi
usubirie barabarani basi linalokwenda huko umpe dereva barua yako na kule ndugu
yako asubirie stendi ya mabasi kupokea ujumbe huo?. Kwan si atakuwa ujumbe
kapata kwani lazima umpigie simu? mbona wazee wetu walitumia njia hiyo wewe
kinachokushangaza ni nini? Kwanza utakuwa umekwepa gharama za kununua vocha.
Ebo,
serikali na bunge kwa ujumla mmekera sana. Mnaturudisha zama gani? Mnachoifanyia
nchi hii walah ni ujambazi wa mchana kweupe peee. Waziri anasimama anasema
kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja ni gharama saaaana ambayo serikali
haiwezi kubeba. Halafu baada ya miezi kadhaa tunamuona katibu wa bunge akiingia
Ikulu na mfurushi wa mapesa anamwambia Rais “Mheshimiwa haya mafurushi ya pesa
yamebaki” Ebo!! Si mmesema hakuna fedha nyie za kulipia matangazo? Hizo zimebaki
wapi?. Wakati huo huo wapo wanaosema mbona hapo nyuma hatukuwa tunarusha
matangazo moja kwa moja sasa mimi naomba warudi nyuma pia kwa kuacha kutumia
simu kwa mawasiliano halafu tuone “hiyo nyuma” ina ubaya gani.
Sasa
kuna hawa wanaotia kichefuchefu wanaosema mbona hata mataifa ya magharibi
hawarushi moja kwa moja, alaa! Basi na sie tuanze kuoana wanaume kwa wanaume
ili twende sawa na mataifa ya magharibi. Yani sisi hatuna la kuwafunza wao
eeh.Kuwa kiiila chao ni chema sio, ebo.
Haya, serikali
inatuambia lipa kodi lipa kodi lipa kodi asielipa kodi anaiibia serikali na
sisi tunatii tunalipa kodi ikifika wakati wa kupangia matumizi hizo kodi loh!
Mnataka mjifungie gizani. Huu ni ujambazi.Kwanini hamtaki tuone na kufatilia
mnayojadili?mnaogopa nini?kwanini mnakimbia kivuli chenu wenyewe. Serikali
inataka kuturudisha enzi za ujima, HAPANA hii si sawa hata kidogo. Katika zama
hizi hatuwezi rudi tena huko nyakati za kuletewa habari zilizoghoshiwa.
Niwasihi
serikali na bunge kwa ujumla mturudishie matangazo ya bunge ya moja kwa moja.
Tunataka tuwaone wawakilishi wetu bungeni wanasema nini,kitu gani kimejadiliwa
na serikali imejibu nini. Huo usiku wa manane mnaotaka tuangalie vipindi
mlivyoviediti ili tuchelewe kulala na asubuhi mnatuwekea madaftari getini ya
kusaini na kutupigia mistari miekundu tukichelewa hatutaki.
0 comments:
Post a Comment