Ndoa nyingi huvunjika, na wapenzi wengi
huachana kabla hata hawajafunga ndoa. Kabla ya ndoa kuvunjika na wapenzi
kuachana hutokea visa vingi vya usaliti, ukigeugeu na chuki. Mapenzi nini?
Mahala pake hasa ni wapi? Asili yake wapi?Wakati gani usaliti hutokea? Wakati
gani mtu anakuwa kigeugeu? Nini hasa chanzo cha chuki kwa wapenzi?
Hakuna maana moja ya mapenzi, ila
vyovyote iwavyo mapenzi ni ile hali ya kuvumilia na kukubali mapungufu, udhaifu
na karaha za mtu yoyote au hali yeyote au kitu chochote. Mapungufu, udhaifu na
karaha zinapokuwa za kiwango kikubwa na bado ile hali ya uvumilivu na kukubali
ikaendelea kuwepo,basi hapo ujue kuwa kiwango cha mapenzi kiko juu sana, na
kinyume chake ni kweli. Ukiona mtu yuko na mapungufu na mbaya zaidi ni kero
kwako lakini bado wampenda basi ujue kuwa uko na mapenzina huyo mtu.
Mapenzi mahala pake ni moyoni; ambapo si
lile pande la nyama lenye vyumba na mishipa ya kutoa na kuingiza damu, bali ni
ile roho ambayo ndio asili ya nguvu zote zinazopatikana ndani ya mwili wa
mwanadamu. Mwili wa mwanadamu tunaweza kufananisha na kompyuta.
Kopyuta imeundwa na mifumo miwili yenye
kutegemeana ambavyo ni hardware na software. Vile vitu tunavyoweza kuvishika na
kuviona ndio hardware na vile ambavyo hatuwezi kuviona wala kuvishika ni
software. Software ndio huilazimisha hardware nini ifanye, na hardaware hupokea
command toka kwa software.
Kwa upande wa mwanadamu kuna roho na
mwili. Roho ndio huamuru kitu cha kufanya na katu mwili hauwezi kuiamuru roho
kitu cha kufanya. Roho ni kama OS[Operating System] kwa kompyuta.
Kwa mujibu wa mapokeo ya dini za
kikristo na kiislamu, mwili wa mwanadamu umeumbwa kutokana udongo, kisha mungu
akupulizia pumzi yake kwenye hilo dongo hata likawa mwanadamu mwenye uhai.
Kama nilivyosema awali kuwa roho ni kama
OS, na ndani ya OS huweza kuongezwa programu mbalimbali kulingana na uhitaji wa
mtumiaji wa kompyuta, pia kwa mwanadamu pia huwa kuna viprogramu vidogodogo
vinavyopatikana ndani ya ROHO.
Viproglamu hivyo vidogo vidogo ni kama
vile vya kucheka,kununa, kuchukia, kutamani, kupenda, nk, Kila ROHO si lazima
iwe na viprogramu hivi vyote, bali zingine huwa na hizi na hukosa zile na
zingine hupata zile na hukosa hizi. Kikubwa cha kufahamu ni kuwa mwanadamu
hawezi kucheka kama hana hicho kiprogramu cha kumuwezesha kucheka, kama vile
huwezi kuchezesha video kwenye kompyuta yako kama hauna programu ya kukuwezesha
kuchezesha video. Watu wengine hawajui kununa na wengine hawajui kucheka pia,
hiyo ni kwasababu hakuna kitu hicho cha kununa au kucheka kwenye roho zao.
Upendo na chuki ni moja kati ya viprogramu vilivyopo kwenye roho.
SOUL
MATE. Class mate humaanisha ni mtu ambaye
umesoma naye darasa moja, naam, mlikutana huko darasani. Nini maana ya SOUL
MATE? Hivi roho hukutana? Kwa mujibu wa dini ya kiislamu M/Mungu alianza
kuziumba roho za viumbe vyote kabla hata ya kuumbwa ulimwengu na ziliishi miaka
mingi kabla hata hazijatiwa au kupuliziwa kwenye miili ya viumbe hivyo. Hivyo
basi huenda hizo roho zilikutana huko kwa mara ya kwanza.
Katika filamu ya kihindi inayoitwa Dil
To Pagal Hai mtunzi ametueleza kuwa roho zimeumbwa katika jozi, yaani mbili
mbli huku zikiwa zimenatana. Wakati wa kutiwa kwenye miili ya viumbe
zikatenganishwa, moja ikatiwa kwa mwanaume na nyingine ikatiwa kwa mwanamke.
Hizi roho mbili lazima zikutane, na kukutana kwenyewe ni kwa watu waliobeba
roho hizo kuoana, na ndoa iliyofungwa na watu wenye hizi roho mbili[soulmate]
katu hawawezi kuachana.
Usaliti? Kigeugeu? Mara baada ya M/Mungu
kupulizia pumzi yake kwenye mwili wa mwanadamu, baadaye na hii mara baada ya
kutokea uasi mbinguni zikaingia pumzi zingine ngeni kwenye miili ya wanadamu.
Pumzi hizi ni majini, au mashetani au mapepo. Hizi pumzi hufanya kazi kama roho
ndani ya mwili. Nilisema huko juu kuwa roho huamuru mwili cha kufanya, hivyo na
haya majini pia huamuru mwili cha kufanya.
Mkumbuke Hawa na Adamu hawakuwahi
kufikiria japo kuusogelea ule mti wa kati, lakini baada ya pumzi mpya kumuingia
hawa, si kwamba waliusogolea tu, lakini pia wakala na lile tunda. Roho ya mtu
iliumbwa kwa mfano wa Mungu, na kiasilika haiwezi kutenda dhambi au kuacha
kumtii Mungu, ila roho ngeni zilizo muingia ndio humfanya atende dhambi, ndio
maana twaambiwa kuna pepo la uzinifu, uongo, wizi, na kubwa zaidi roho zetu
halaumiwi kwa kutenda dhambi bali zinalaumiwa kwa kushindwa vita na shetani.
Kwakuwa ndani ya mwili tayari kuna roho,
na kwakuwa hizi roho ngeni[majini] nazo huamrisha mwili, hivyo basi huwa
panatokea mashindano mengi ya kiroho ndani ya mwili wa mwanadamu. Vita.
Mwili siku zote hutii ile roho
iliyoshinda haijalishi hiyo roho ni ngeni au ile aloumbiwa mwanadamu. Mfano
mwanadamu waweza kutoka kuoga kisha ukajikuta uko katika mtihani wa kuchagua
nguo ya kuvaa, wakati mwingine waweza kuvaa nguo kabisa kisha ukajikuta waivua
na kuivaa nyingine, ila hali ya kuchagua nivae hii au ile ni matokeo ya
mashindano ya kiroho ndani ya mwili, Vita.
Hata katika kuchagua mpenzi pia hutokea
mashindano ya kiroho ndani ya mwili. Unapochagua mpenzi na kuamua kuishi naye
jua kuwa kuna roho imekushinikiza kufanya hivyo na si vinginevyo. Kwakuwa watu
wote tuko na roho ngeni nyingi kwenye miili yetu, kwakuwa hizi roho
hutofautiana nguvu kulinganana nyakati, na kwakuwa roho yenye nguvu kwenye
wakati fulani ndio hutawala kipindi hicho, hivyo basi kiwango cha “mapenzi” ya
mwanadamu kwa mwenza wake hubadilika kadiri roho zinazotawala mwili wa
mwanadamu huyo zinavyobadilika;hapa ndipo usaliti na kigeugeu vinapozaliwa.
Wakati wampenda mwajuma elewa kuna
kiprogramu[roho] ndani ya mwili wako kimekufanya umpende huyo mwajuma, hiyo
roho ikizidiwa nguvu hata ikaingia roho ya kumpenda Asha lazima utamuacha
mwajuma na kuanza kumpenda Asha. Hizi roho ngeni ndio hupelekea “soulmate”
wakati mwingine zisikutane. Kama ile roho ya inayompenda Asha ikiendelea
kutawala kwa muda mrefu hata mauti, basi huyo mtu atendelea kumpenda Asha hadi
kifo chake.
Cha kuzingatia, ile roho inayomfanya
John ampende Asha haiwezi kufaulu hadi Asha awe na roho inayompenda John. Ikiwa
roho hizi ni "SOULMATE" basi mapenzi ya Asha na John hudumu daima,
kama hizi roho si "soulmate" na hivyo mapenzi yao ni matokeo ya roho
ngeni[majini] zilizopendana, kwa hivyo mapenzi hayo yatachuja na kupotea kabisa
mara baada ya roho hizo kutolewa kwenye utawala na roho zingine.
Roho ngeni namaanisha majini au mapepo.
Kila mwanadamu ana majini wengi na kila jini kuna mambo anapenda na kuna mambo
anachukia, na kila jina kuna siku yake, mwaka wake na hata muongo wake wa
kutawala. Pia kila jini ana nguvu zake za kikawaida alizoumbwa nazo na kuna
majini wengine wana nguvu za ziada(uchawi)
MWISHO:
katika yote hayo juu, naomba rejea
kitendo cha Kefa kumkana Yesu mara tatu, rejea usaliti wa Yuda Iskariote kwa
Yesu, rejea vita vya maswahaba baada kifo cha Mtume Muhammad(s.a.w), pia rejea
maisha yako kila siku. Utabaini bila jelezi kuwa usaliti, kigeugeu, mapenzi,
urafiki, nk vinatawaliwa na majini na roho, na kwasababu hiyo miili yetu haina
hiyari hata kidogo.
Siku nyingine nitafafanua uhusiano kati
ya majina yetu na mahusiano mapenzi na ndoa. Kwanini watu wengine huchezesha
herufi za majina yao au hubadili majina kabisa kwa lengo la kuimarisha ndoa na
mahusiano.
0 comments:
Post a Comment