Si
mara moja na inajulikana fika kuwa kuongezeka kwa pato la
taifa sio kupungua kwa idadi ya maskini katika nchi. Hii inajulikana kuanzia na
wachumi hata viongozi wa mataifa hayo kuwa pato la nchi laweza ongezeka lakini
ikawa ni kwa sababu ya mchango wa watu wachache tu wanaomiliki uchumi wakati
walio wengi wakabaki hohehahe. Hivyo njia bora ya kupima maendeleo ni kuangalia
vipimo vya kijamii kama vile upatikanaji wa huduma bora za afya,maji safi na
salama, makazi bora, chakula, elimu bora na mambo kama hayo.
Katika
ripoti ya Kutathmini umaskini wa Afrika “Africa
Poverty Report” iliyoandaliwa na Kathleen Beegle, Luc Christiansen, Andrew
Dabalen na Isis Gaddis waliyoiita “Poverty
in a Rising Africa”(Umaskini katika Africa inayoamka) wameweka bayana kuwa
watu wengi sasa hivi ni maskini ukilinganisha na mwaka 1990. Mwaka 1990 watu
milioni 280 walihesabika kama maskini lakini mpaka kufikia mwaka 2012 watu 380
walikutwa ni maskini labda hii inatokana na ongezeko la watu.
Ripoti
inaonyesha pia kuwa uchangiaji wa bara la Afrika katika umaskini wa dunia
umepungua kutoka asilimia 56 mwaka 1990 mpaka asilimia 43 mwaka 2012. Gepu kati
ya umasikini wa mijini na vijijini pia limekuwa likipungua japo bado sehem
kubwa vijijini ni maskini sana. Ripoti inaonyesha pia kuwa kati ya watu wazima 5
basi 2 bado hawajaelimika
Bado
tatizo la usawa ni changamoto Afrika ambapo kati ya nchi kumi duniani ambapo
hakuna usawa basi nchi saba zinatoka Africa hasa kusini mwa jangwa la sahara.
0 comments:
Post a Comment