SHIRIKA la
Fedha la Kimataifa (IMF) limetoa ripoti kuhusu mustakabali wa uchumi wa dunia,
likibatilisha makadirio ya awali lililotoa Januari mwaka huu kuhusu mwelekeo wa
ukuaji wake.
Awali,
mapema mwaka huu, IMF ilisema uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 3.4 mwaka huu
na asilimia 3.6 mwaka ujao.
Lakini kwa
mujibu wa ubashiri wake mpya uchumi huo utakua kwa asilimia 3.2 mwaka huu na
asilimia 3.5 mwaka 2017 likitahadharisha kuwa unakabiliwa na hatari ya kutoongezeka.
Licha ya
hilo, IMF imepandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka huu na
mwakani hadi asilimia 6.5 na asilimia 6.2.
Baada ya
mashirika maarufu ya Marekani ya kutathmini uwezo wa nchi kuhimili madeni ya
Moody’s na Standard & Poor’s kushusha hadhi ya China kwenye tathmini zao,
ripoti hiyo mpya inatarajia kuongeza imani ya watu na mustakabali wa ukuaji wa
uchumi wa China.
Mchumi Mkuu
wa IMF, Maurice Obstfeld, anasema uchumi wa dunia unaendelea kufufuka, lakini
kasi yake ni ya taratibu mno na inasikitisha watu na kwamba itasababisha ukuaji
wake kukabiliwa na hatari nyingi zaidi.
Ukuaji
taratibu wa uchumi wa dunia umedumu kwa muda mrefu sasa.
Kwa mujibu
wa makadirio mapya kuhusu mustakabali wa uchumi wa dunia, ikilinganishwa na
hali ya mwaka 2015, ongezeko la uchumi huo kwa mwaka huu litakuwa ni asilimia
3.2 tu, na mwakani litafikia asilimia 3.5.
Obstfeld
alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne wiki
mbili zilizopita mjini Washington, Marekani, ambapo ripoti kuhusu mustakabali
wa uchumi wa dunia ilitolewa hadharani.
Kwenye
hotuba yake, Obstfel alitoa tahadhari kuhusu ufufukaji wa taratibu na udhaifu
wa uchumi wa dunia na kusema kupungua kwa ongezeko la uchumi kunaweza kupunguza
thamani ya sarafu duniani, kuchochea utaifa na kusababisha migogoro ya siasa za
kijiografia.
0 comments:
Post a Comment