SIMBA NA AZAM HAKUNA MBABE TAIFA
Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo hii kwa kuzikutanisha Timu za Simba yenye masikani yake pale Kariakoo Msimbazi na timu ya Azam Kutoka Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliokuwa wa mashambulizi ya kushtukiza kwa pande zote mbili umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana huku ikishuhudia timu zote zikikosa nafasi za wazi za kufunga.
Kwa matokeo hayo Simba inabaki Nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia pointi 58 baada ya kucheza michezo 26. Azam nayo inakamata nafasi ya pili kwa kupata alama 59 baada ya mechi 26 na Yanga imebaki k=ikijitanua kileleni kwa kujikusanyia jumla ya alama 65 baada ya mechi 26.
Yanga Ana Nafasi Kubwa Sasa Kuchukua Ubingwa, Ila Kule KWenye FA, Kati ya Yanga na Azam Mhh mtoto hatumwi dukani
ReplyDelete