Inaweza ikawa ni harufu ya jipu jipya katika ofisi ya
Makamu wa Rias (Mazingira) baada ya wabunge kuhoji kulikoni fedha zilizotolewa
na wafadhili kwa ajili ya miradi ya mazingira katika maeneo ya Dar es Salaam,
Bagamoyo, Pangani, Rufiji na Zanzibar Zaidi ya shilingi bilioni tisa kuombwa
tena katika bajeti ya mwaka huu. Wabunge wamehoji kulikoni kiasi hicho cha
fedha kiombwe kwa ajili ya kazi hiyohiyo wakati tayari wahisani Marekani na
Ujerumani tayari walishafadhili mradi huo.
Kwa mujibu wa wabunge wakiongozwa na
kambi ya upinzani, miradi hiyo miwili ilikumbwa na ufisadi mkubwa ambao ulikuwa
ukiendeshwa baina ya mtumishi mmoja aliyeko katika Ofisi ya Makamu wa Rais
Idara ya Mabadiliko ya Tabianchi akishirikiana na kigogo mmoja aliyekuwa Ikulu
wakati wa utawala wa awamu ya nne.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri Kivuli katika Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira), Pauline Gekul wakati akiwasilisha taarifa ya kambi
hiyo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi katika ofisi hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/17.
“Mtumishi huyo wa Serikali alishirikiana na kigogo mmoja aliyekuwa Ikulu
wakati wa utawala wa awamu ya nne katika kutafuna fedha ambazo zilikuwa
zimetolewa na wafadhili,” alisema Gekul.
Kutokana na kashfa hiyo aliitaka Ofisi ya Makamu wa Rais imtake Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanyie ukaguzi maalumu (Special
Audit) wa miradi hiyo miwili.
“Tunataka CAG akague miradi hii ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi
, pamoja na miradi mingine yote iliyosimamiwa na Kitengo cha Mabadiliko ya
Tabianchi kilichopo chini ya Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais,
kwani kuna majipu ya kutumbua.
“Tunaomba Bunge lisitishe kupitisha maombi ya fedha ya mradi huu hadi
ukaguzi maalumu utakapofanyika kuhusu fedha za mradi ambazo zilikuwa zimetolewa
na wafadhili utakapokamilika,”alisema.
0 comments:
Post a Comment