Mgombea urais anayeonekana kuongoza katika kinyang’anyiro cha kumteua
mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amekataa kushiriki mdahalo
dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders.
Maafisa wake wa
kampeni wamesema badala yake, Bi Clinton ameonelea ni heri kukabiliana na
mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump kuliko kupoteza muda huo
kufanya mdahalo na Bw. Sanders.
Bi Clinton alikuwa
awali amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo
la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.
Bw Sanders, Seneta wa
Vermont, amesema hajashangazwa na uamuzi huo wa mpinzani wake.
Wapo wachambuzi
wanaodai labda uamuzi huo wa Bi. Hillary ni kutotaka kuharibiwa na Bw Sanders
anaeonekana kuwa mwiba mkali katika midahalo ama ni kwa sababu ameona anaongoza
hivyo ni afadhali ajipange kukabiliana na mgombea wa Republican Bw Trump
anaeonekana ndie atakayepitishwa na chama chake katika kinyang’anyiro hicho.
Na katika hatua
inayoonesha viongozi wa Democratic hawataki kumtenga Bw Sanders na wafuasi
wake, wametangaza kwamba mgombea huyo ataruhusiwa kuteua theluthi moja ya
kamati ya kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwezi Julai.
Mkutano huo hutumiwa
kuidhinisha mgombea urais wa chama cha Democratic.
Uchaguzi mkuu nchini
Marekani utafanyika mwezi Novemba.
0 comments:
Post a Comment