Benazir Bhutto |
Historia yake ni
ndefu hata kunyongwa kwa baba yake ambae nae aliwahi kuwa waziri mkuu wa taifa
hilo. Ndoto za mwanaharakati huyu zilizimwa rasmi mchana siku ya tarehe 27
Desemba 2007 mjini Rawalpindi Pakistani akitoka kuhutubia mkutano wa kampeni
katika uwanja wa Liaquat National Bagh. Ikumbukwe ni katika kampeni ambazo
uchaguzi wake ulikuwa umepangwa kufanyika
January ya mwaka unaofuata yaani 2008. Yeye akiwa anapeperusha bendera ya
chama kikuu cha upinzani na kilichokuwa na nguvu cha Pakistan People’s Party
dhidi ya chama alichokuwa akikiongoza Rais wa wakati huo Gen.Perves Musharraf. Taifa la Pakistan
liliingia simanzi majira ya saa 12:16 jioni katika hospitali ya Rawalpind baada
ya Bhutto kufariki dunia.
Nini Kilimuua?
Kwanza ikumbukwe
Benazir Bhutto akiwa anatoka kuhutubia bomu lilimlipukia kwenye gari alilokuwa
akilitumia na hivyo kunusurika na kukimbizwa hospitali. Mara baada ya kufariki
waziri wa mambo ya ndani alitoa ripoti kuwa Benazir amefariki kutokana na
mpasuko katika ubongo (Brain Fructure). Lakini ni hapo wasaidizi wa Benazir
walipovunja ukimya kuwa si kweli Benazir mbali ya bomu lile lakini alipigwa
risasi mbili na mtu asiejulikana. Wakitoa ushahidi huo Rais Perves Musharraf
aliingilia kwa kusema wasaidizi wale ni waongo na wazushi lakini baadae
madaktari waliokuwa wamezuiwa kusema chochote waliamua kukiri kuwa ni kweli
Benazir alipigwa risasi hivyo kumlazimu waziri kutengua kauli yake ya mwanzo.
Ni hapo Perves Musharraf alipoanza kuhusishwa na sakata hili.
Baitullah Mehsud
ndio hasa muuaji wa Bi.Benazir Bhutto na si Musharraf. Japo kwa sasa Musharraf
anahesabika kama muuaji na mpangaji wa kifo cha Bhutto lakini taasisi ya
kiitelijensia ya Pakistan (Inter-service Intelligence of Pakistan) ambayo ni ya
kwanza duniani kwa inteligensia ikifuatiwa na CIA ya marekani zote kwa kushirikiana
zinakiri kuwa Baitullah Mehsud kiongozi wa kikundi cha Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) chenye uhusiano na Al-Qaeda ndiye
hasa aliepanga mkakati huu.
Mkurugenzi mkuu wa
CIA Gen.Michael Hyden amenukuliwa akisema “Mpango
huu umefanywa na mtandao wa Baitullah Mehsud. Hakuna shaka katika hilo”.
Hii ni baada ya kupatikana kwa mawasiliano ya simu kati ya Baitullah na
waliotega bomu na kumpiga risasi Benazir wakati Baitullah akiwapongeza kwa kazi
hiyo.
Perves Musharraf |
Kwanini Musharraf ahusishwe?
Kwanza Musharraf
hakuwa na namna na inawezekana alipatwa na kiwewe. Anahusishwa kwa sababu ni
yeye wa kwanza kabisa kumpigia simu Bhutto na kumtaka asirudi Pakistan kuja
kugombea baada ya Bhutto kukaa uhamishoni kwa miaka tisa kwa sababu za kisiasa.
Ikumbukwe Musharraf alikuwa ni mkuu wa majeshi mstaafu wa jeshi la Pakistani na
alikuwa na uongozi wa kiimla (Dictator) na mpinzani mkubwa wa Benazir. Benazir
alikataa na kuamua kurudi na kulakiwa na maelfu ya wa Pakistan na hivyo
kumuweka pabaya Musharraf katika kurudi tena madarakani.
Pili baada ya
kurudi kwa Bhutto mwaka 2007 alinusurika kuuawa kwa bomu na hivyo alimuomba
Musharraf ampe kibali aagize makampuni binafsi ya ulinzi kampuni ya Black water
na ArmorGroup ya uingereza wasaidie kumlinda (Kwanini aliyaamini makampuni
haya?..tutajadili wakati mwingine). Ombi hilo Musharraf alilikataa. Benazir pia
aliomba gari analotumia liwekwe tintedi lakini serikali ilimkatalia katakata.
Lakini pia siku aliyopigwa risasi vizuia mawasiliano (mobile jammers) hazikuwa
zinafanya kazi.
Sababu kubwa zaidi
ni baada ya kugundulika kuwa kati ya waliohusika na tukio lile watatu ni
“vijana” wa Musharraf na kitendo cha Musharraf kutoka hadharani mara tu baada
ya Bhutto kufariki na kuwaita wasaidizi wa Bhutto kuwa ni wazushi na baadae
madaktari kuthibitisha ilitosha kumwingiza kwenye kashkash hii.
Kwanini Musharraf alimkingia kifua Baitullah?
Labda hiyo iwe ni
habari ya wakati mwingine lakini ikumbushwe tu kidogo kuwa Musharraf na
Baitullah walikuwa ni mahasimu wakubwa hasa kutokana na Baitullah kuongoza
kikundi kilichohesabika kama cha kigaidi na Musharraf na kiliisumbua sana
serikali ya Pakistan tangu Musharraf akiwa mkuu wa majeshi. Wakati huu
Musharraf aliungana na Baitullah kila mtu akiwa na interesti yake binafsi.
Halikuwa wazo la Musharraf kumuua Benazir (ISI na CIA wanaripoti) ila Baitullah
alimlazimisha Musharraf kumkingia kifua. Sababu za hii “cover up” zitaelezwa wakati ujao.
Tangu igundulike
kuwa kuna mtu nyuma ya Musharraf aitwae Baitullah vyombo vya usalama vilianza
kumtafuta bila mafanikio mapaka siku ya tarehe 5/8/2009 ndege ya kivita isiyo
na rubani “drone” ya kimarekani
ilipomlipua na kumuua hapo hapo Baitullah akiwa nyumbani kwa baba mkwe wake
akijiuguza magonjwa ya figo huko kusini mwa Waziristan.
Kwanini Musharraf alikubali kumkingia kifua
Baitullah? Nini kiko nyuma ya huu mlolongo wa mauaji?Mada itaendelea wakati ujao
0 comments:
Post a Comment