Hatimaye Serikali kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo
imetangaza rasmi kusitisha wimbo na video ya muziki wa Chura wa Msanii
Snura Mushi kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya Habari kuanzia leo Mei
4.2016 mpaka pale atakapourekebisha na kuendana na maadili ya Tanzania. Serikali pia imemfungi Snura kujihusisha na masuala ya sanaa ikiwemo
kutumbuiza kwenye matamasha mbalimbali hapa nchini
“Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya
msanii Snuara mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi
zake Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Pia inawataka wasanii kujiuliza
mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa
na marafiki zao watazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha, waelewe
kwamba Sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu hata kidogo..” alieleza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Zawadi
Msalla.
Kufuatia
hatua hiyo wadau wa masuala ya Sanaa wameanza kuhoji iweje video ya wimbo wa
Chura ifungiwe wakati video ya wimbo wa Asanteni kwa kuja wa mwanamuziki
Mwanafalsafa ukiendelea kuwa hewani. Nini maadili ya wimbo wa Asanteni kwa kuja
tofauti na ule wa Chura.Lakini wapo wanaohoji kuwa serikali inataka kuliua soko
la Sanaa nchini kwa kuwafungia wanamuziki katika kazi zao za Sanaa.
0 comments:
Post a Comment