Zitto Aonyesha Ukomavu Kwa Polisi,Ampa Rai Nzito Magufuli




 
Leo Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo amedhihirisha ukomavu wake wa kisiasa sio tu kwa kuitika wito wa jeshi la polisi la kumtaka kwenda kuhojiana nae bali kwa kutoa rai kwa muheshimiwa Rais Magufuli juu ya hatua ya serikali yake kutaka kuwaziba midomo wapinzani nchini.
Akihojiwa kwa saa tatu na Kamanda wa Upelelezi mkoa wa kipolisi wa Temeke na Naibu Kamada wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alisema Mambo kama haya ya kuwanyanyasa wapinzani yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini sasa sote ni mashahidi jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa na kwamba ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia yao.
Jana (Jumanne) jeshi la polisi lilizuia mikutano ya kisiasa mpaka hapo litakapotoa tena taarifa ya kuruhusu mikutano hiyo hatua ambayo Zitto amesema  sio sahihi kwa jeshi hilo kufanya namna hiyo.Kiongozi huyo amenukuliwa akisema ni lazima kama chama cha ACT Wazalendo waende mahakamani kupata tafsiri sahihi ya katazo hilo.
Juu ya kusiginwa kwa demokrasia nchini kiongozi huyo alinukuliwa akisema  “Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana”.
“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu kwa kunihoji tu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.
Zitto amemtaka Rais kuhakikisha serikali yake badala ya kusigina demokrwasia inasaidia kuifanya ichanue na kuwa zama za kuongoza watu kwa vitisho zimepitwa na wakati.

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment