Top 10 Ya Wanamuziki Wa Kiume Wenye Sauti Zenye Mvuto Tanzania Hii Hapa


Tanzania ina vipaji vingi na wasanii wengi wa kiume wanaofanya muziki wa Bongo flavour wa miondoko ya R n B almaarufu  muziki wa kuimba.Kati ya wengi leo tutakuletea wasanii kumi wakali wanaoonekana kuwa na sauti zenye mvuto na za kuvutia kusikiliza nyimbo zao hasa wanapoimba.
Vigezo vilivyozingatiwa ni uwezo wao wa kuimba  kwa pitch zote za juu na za chini na kati,uwezo wao wa kuhimili kuimba kwa muda mrefu bila sauti kuathirika na uwezo wao wa utunzi mwanana.
1.      Ali Kiba
Namba moja anaishikilia Ali Kiba, mwenyewe hujiita King Kiba.Huyu ni mwanamuziki wa siku nyingi na tangu aanze muziki wake sauti yake haikuwahi kuchuja.Huyu huweza kuimba kwa sauti kali sana,kati na hata ya chini bila kukwama wala kukosea.
2.      Barnabas
Anashikilia namba mbili huyu sio uimbaji tu ni mtunzi mzuri sana wa nyimbo na sio za kwake peke yake bali hata wasanii kadhaa wamekiri kutungiwa nyimbo na msanii huyu
3.Ben Pol

Anashikilia namba tatu huyu ana uwezo mkubwa wa kucheza na sauti yake hata ukaburudika haswa.
4.Baraka Da Prince
Huyu ni msanii mpya lakini alieonyesha kutobahatisha hasa kwa sauti yake ya juu mara nyingi na tungo murua za mapenzi.
5.Linex
Hujiita voice of Africa.Huyu sauti yake ni ya kukwaruza ama inayoonekana kutaka kukwama lakini tungo zake hakika utazifurahia.
6.Christian Bela
Mwanamuziki wa muziki wa dansi lakini mwenye kuimba na kutunga nyimbo zisizochuja kusikiliza.Ana uwezo mkubwa sana wa utunzi.
7.Amini
Amini yeye ni mwimbaji mzuri na sauti yake ni ya kubembeleza.Ni zao la THT
8.Peter Msechu
Peter ni mwalimu wa muziki haswa kwa hiyo haishangazi kumwona kwenye orodha hii.Anajitosheleza
9.Diamond Platinums
Huyu anajulikana haswa kwa kucheza na sauti na midundo.Anavuma kimataifa
10.Mo Music

Msanii mpya lakini pindi usikilizapo tungo zake na sauti yake utakubaliana nasi kuwa anastahili kuingizwa kwenye list hii.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment