Je, Kafulila Atarudishwa Bungeni Kesho?


Ferdinand Wambali Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora anatarajiwa kutoa hukumu ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini kesho tarehe 17 Mei.Katika kesi hiyo iwapo David Kafulila aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge kupitia NCCR-Mageuzi atashinda basi ataruingia bungeni rasmi.
Kesi hiyo ya kupinga matokeo ilifunguliwa na David Kafulila aliyekukuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi dhidi ya mpinzani wake Husna Mwilima wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayedaiwa kupoka ushindi wa Kafulila.
 
Wambali anayesimamia kesi hiyo katika taarifa yake iliyotolewa siku ya jumatano tarehe 4 mwezi huu mjini Tabora amesema kuwa, amepanga kutoa hukumu kesho baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao
Awali, Jaji Wambali aliamuru Mwilima kuwasilisha ushahidi uliompa ushindi lakini pia msimamizi wa uchaguzi huo naye apeleke ushahidi uliomfanya ampe ushindi Mwilima.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Wambali aliomba kupatiwa muda wa kutosha ili kupitia ushahidi huo na vielelezo vilivyowasilishwa ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi mpinzani wake   Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo kwa mujibu wa kura zake.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na, Mbunge wa jimbo hilo, Mwilima , Mfaume, na Mwanasheria wa serikali anayewakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ktika kesi hiyo wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Mwilima huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu Prof. Abdallah Safari,Tundu LissU na Daniel Rumenyela.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment