Bajeti Za Afrika Ya Mashariki 2016/2017.Elimu, Ajira,Miundombinu,Nishati Na Kilimo



 
Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Ya Mashariki wameamua kuimarisha chumi za nchi zao kwa kuimarisha sekta za miundombinu na nishati.Katika bajeti zao zilizowasilishwa jana, Kenya ambayo ndio inaongoza kwa uchumi mkubwa  imepanga kutumia dola za kimarekani 22.8 bilioni wakati Tanzania imekadiria dola bilioni 13.5, Uganda dola bilioni 12 huku Rwanda ikikadiria dola bilioni 2.49 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Burundi yenyewe haipo kwenye utaratibu huu wa kusoma bajeti kwa pamoja.

TANZANIA

Dr.Phillip Mpango
 
Akiwakilisha hotuba ya bajeti Waziri wa Uchumi na Mipango Phillip Mpango ameainisha kuwa bajeti hii mpya itajikita katika kupambana na changamoto za mwananchi wa kipato cha chini na kuweka misingi imara ya uchumi kwa ajili ya wale wa kipato cha kati.Katika nchi ambayo deni la taifa ni dola za kimarekani bilioni 20.94 mpaka kufikia Machi mwaka huu shunguli za maendeleo zimetengewa asilimia 40.

Pia Tanzania imepanga kukopa shilingi trilioni 7.4 kutoka katika pato la ndani ili kuziba mwanya katika mwaka huu wa fedha.Serikali pia itatumia shilingi trilioni 17.7 kama pesa za kuendeshea shuguli za kila siku na shilingi trilioni 11.8 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Katika hilo zaidi ya shilingi trilioni 4.77 sawa na asilimia 22.1 zimeelekezwa katika elimu.Waziri pia akatangaza ongezeko la kodi kwa mvinyo na bia.Zaidi ya shilingi trilioni 18.4 sawa na asilimia 62.5 ya bajeti imepangwa kupatikana kwa makusanyo ya ndani.

KENYA

 
Henry Rotich
 
Kwa upande wa kenya waziri wa fedha wa nchi hiyo Henry Rotich amesema katika bajeti ya mwaka huu itajielekeza kwenye miundombinu na kilimo.Waziri akafuta kodi juu ya chai na sukari.Sekta ya nishati ikapatiwa shilingi za kenya bilioni 39.9,reli ya kisasa ikatengewa shilingi za kenya bilioni 228.5 na barabara shilingi za kenya bilioni 147.6

UGANDA

Matia Kasaija
 
Uganda yenyewe bajeti yake itajikita katika kuimarisha sekta ya nishati na miradi ya miundombinu ya usafirishaji.Lakini pia itajikita katika sekta ya kilimo hasa kukifanya cha kisasa na kuongeza mazao thamani ili yawezwe kuuzwa soko la nje..Waziri wa fedha wa nchi hiyo Matia Kasaija alisoma hotuba hiyo yenye makadirio ya shilingi ya uganda bilioni 26,361,alisema kuimarisha biashara ya mafuta na gesi ndio itakuwa kipaumbele cha kwanza kwa mwaka wa fedha ulioanza na hivyo serikali imetenga shilingi ya Uganda bilioni 188.2 katika kukamilisha azma hiyo.

Hata hivyo sehemu kubwa kabisa ya bejti ya mwaka huu ya Uganda imeelekezwa kwenye wizara ya ajira kwa kutengewa shilingi ya Uganda trilioni 3.7 ikifuatiwa na sekta ya elimu iliyopata shilingi ya Uganda trilioni 2.7 na sekta ya nishati trilioni 2.4

Waziri huyo pia aliongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi ya Uganda bilioni  343.46 mwaka jana mpaka bilioni 823.42 mwaka huu ili kuongeza uzalishaji na biashara ya mazao ya kilimo.

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment