“Apps” 10 Za Simu Zilizofanikiwa Zaidi Duniani


 
#10 Yahoo Stocks

 
Duniani sasa hivi wengi wanapenda kuwekeza kwenye masoko ya hisa.Tofauti na miaka ya nyuma ambapo si wengi wa rika la ujana walipendezwa na biashara hii sasa hivi hata vijana wanajihusisha na uwekezaji wa aina hii.Basi apps hii imachukua nafasi kuliko unavyoweza kudhani.
#9 Apple Maps
 
Apple Maps inashika namba tisa.Ni application nzuri sana inayokuonyesha dira na uelekezi popote duniani.
#8 Instagram
 
Labda hii watanzania wengi wangedhani ndio inayoongoza maana ndio tumejikita huku lakini ukweli ni kuwa inashikilia namba nane.Watu wanapenda kujipiga picha sana basi Instagram ndio penyewe katika kupost vitu vya namna hiyo.
#7 Gmail

Hata hii si ngeni na sijui kama kuna mtu yupo kwenye mtandao wa internet na hana account ya gmail itakuwa ni kioja.Shangaa inashika namba saba.
#6 Google Maps
 
Yani ni waafrika tu ama watanzania ndio hatutumii sana hii application lakini kwa nchi za wenzetu hii inatumika kuliko hata Instagram.Inashika namba sita.
#5 Pandora Radio
 
Hapa Tanzania watu hawaijui ama kama wanaijua basi ni wachache.Hii application unaweza kusikiliza muziki wowote bure.Ijaribu uone utamu wake.
#4 Google Search
 
Hivi kuna mtu ana smart phone na hakuwahi kutafuta chochote kwa kutumia google?.Hii aihitaji maelezo.Ipo namba 4.
#3 Google Play Store
 
Wo wo wo Hii haitaki nieleze sana yani ili upate apps kirahisi sasa hivi ni lazima uingie hapa.Hii inashika namba tatu
#2 YouTube
 
Unataka kutazama video?kusikiliza muziki?kuangalia clips mbalimbali za jambo lolote lile?Unaachaje kuifaham YouTube sasa?Ni apps ya pili duniani kwa kutembelewa na mafanikio.
#1 Facebook
 
Sidhani kama utashangaa kusikia kuwa facebook ndio inashikilia namba moja kwa kutembelewa na watu wengi duniani.Hakika ina haki hiyo.Hii ndio kiboko yao.
 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment