UMASKINI WAPUNGUA AFRIKA HUKU MASKINI WAKIONGEZEKA

Si mara moja na inajulikana fika kuwa kuongezeka kwa pato la taifa sio kupungua kwa idadi ya maskini katika nchi. Hii inajulikana kuanzia na wachumi hata viongozi wa mataifa hayo kuwa pato la nchi laweza ongezeka lakini ikawa ni kwa sababu ya mchango wa watu wachache tu wanaomiliki uchumi wakati walio wengi wakabaki hohehahe. Hivyo njia bora ya kupima maendeleo ni kuangalia vipimo vya kijamii kama vile upatikanaji wa huduma bora za afya,maji safi na salama, makazi bora, chakula, elimu bora na mambo kama hayo.

Katika ripoti ya Kutathmini umaskini wa Afrika “Africa Poverty Report” iliyoandaliwa na Kathleen Beegle, Luc Christiansen, Andrew Dabalen na Isis Gaddis waliyoiita “Poverty in a Rising Africa”(Umaskini katika Africa inayoamka) wameweka bayana kuwa watu wengi sasa hivi ni maskini ukilinganisha na mwaka 1990. Mwaka 1990 watu milioni 280 walihesabika kama maskini lakini mpaka kufikia mwaka 2012 watu 380 walikutwa ni maskini labda hii inatokana na ongezeko la watu.

Ripoti inaonyesha pia kuwa uchangiaji wa bara la Afrika katika umaskini wa dunia umepungua kutoka asilimia 56 mwaka 1990 mpaka asilimia 43 mwaka 2012. Gepu kati ya umasikini wa mijini na vijijini pia limekuwa likipungua japo bado sehem kubwa vijijini ni maskini sana. Ripoti inaonyesha pia kuwa kati ya watu wazima 5 basi 2 bado hawajaelimika


Bado tatizo la usawa ni changamoto Afrika ambapo kati ya nchi kumi duniani ambapo hakuna usawa basi nchi saba zinatoka Africa hasa kusini mwa jangwa la sahara.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment