DIAMOND NA ZARI KIMENUKA

Kama si leo basi kesho tutasikia kuvurugana rasmi kwa mastaa mawili Diamond na Zari ambao mapenzi yao yaliteka vichwa vya habari vya wapenzi wa burudani nchini. Inasemekana na kuhakikishwa na watu wa karibu wa mastaa hao kuwa hawapo “in good terms” na kwamba muda wowote tutasikia la kusikia.

Hii inatokana na Zari kufuma maongezi ya Diamond na msichana mmoja (jina tunalihifadhi) kwenye simu yake yanayoonesha kuwa ni watu waliopo kwenye mahusiano kwa muda  mrefu. Baada ya Zari kumuuliza Diamond katika hali ya kutaka kujua ukweli ili yaishe Diamond alikiri na kusema ilitokea wakati Zari alipojifungua na kwamba hataendelea nae ndipo hapo Zari alipoamua kukiwakisha.

Mama wa Diamond alipojaribu kusuluhisha Zari alimrushia maneno machafu yaliyomfanya mama huyo kukasirika na kulalamika kwa mwanawe Diamond kuwa Zari kamkosea adabu. Mpaka sasa tayari mama wa Diamond ameshafuta picha zote za Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram kuonyesha yupo serious kuhakikisha mwanae haendelei na mahusiano na binti huyo.

Jokate ana nuksi gani?
Katika wasichana wazuri na warembo nchi hii basi Jokate hataachwa kutajwa.Lakini ajabu ni kuwa binti huyu hajawahi kukaa na mwanaume zaidi ya mwaka mmoja. Tulianza kusikia akitoka na mcheza kikapu maarufu Hasheem Thabiti mara wakabwagana, akaamia kwa Diamond wakabwagana akaruka kwa mwana FA nae akabwaga manyanga akahamia kwa King Ali Kiba nae akajitoa hivi majuzi. Shida ni nini na dada huyu?.Ni kuwa hawa wanaume wote hawajui kupenda, hawamridhishi ama nuksi tu?.

Ajabu ni kuwa mahusiano hayo yote achilia mbali yale ya siri hayajawahi kudumu zaidi ya mwaka mmoja ni miezi mitatu mpaka kumi inakuwa nukta. Mtandao huu unatafuta nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wanaume hao na Jokate mwenyewe watueleze kulikoni?



Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment