LEICESTER CITY MABINGWA LIGI KUU UINGEREZA


Bao la Eden Hazard la dakika ya 83, litakuwa bao la historia katika klabu ya Leicester City. Likiwa ni bao la kusawazisha la Chelsea na kufanya matokeo kuwa 2 - 2 dhidi ya Totenham.

Goli hili limefuta kabisa ndoto za Totenham kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu huu. Totenham walitangulia kufunga dakika ya 35 na 43 kwa magoli yaliyofungwa na H.Kane na H.Son.

Dakika ya 58, G. Cahili akaifungia Chelsea goli la kwanza kabla ya Eden Hazard kufunga goli la kusawazisha na kufuta ndoto za Totenham kutwaa ubingwa huku Kukaipa Leicester City nafasi ya kutangazwa Mabingwa wa ligi hiyo yenye msisimko duniani.

Leicester wanaandika rekodi ya kipekee na hii ikiwa ni mara yao ya kwanza kutwaa taji hilo. Ikumbukwe kuwa msimu ulioisha Leicester City walikuwa wakigombea nafasi ya kutokushuka daraja.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment