Tamasha La Picha Za Utupu Lafana Huko Uingereza



Mamia ya watu wamevua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza.
Tukio hilo ni la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
 
Washiriki walipakwa rangi ya samawati Jumamosi na kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
 
 

Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery.
 
Picha zilizopigwa zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
 
Tunick, anayetoka New York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
 


 
Amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany.
 
Bw Tunick amesema kazi zake “hugusia historia ndefu ya Sanaa ya utupu”.
 
"Mavazi ni Sanaa ya mtu mwingine,” anasema.
 


 
“Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake.”
 
Watu karibu 3,000 walihudhuria kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi Machi.

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment