YAMETIMIA: Moise Katumbi Ahukumiwa Miaka 3 Jela


Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.Amesema atakata rufaa
Nini Chanzo Cha Hii Figisufigisu?
Wapinzani na wafuasi wa Katumbi huko Congo wanaiona hii kama komoa komoa ya Rais Kabila dhidi ya Katumbi ambapo hapo kabla walikuwa maswahiba.Uswahiba wao ulianza kuingia doa pale tu Rais Kabila alipotaka kulivunja jimbo la Katanga ambalo ndio kama milki ya Katumbi kiuchumi na kiutawala liwe katika majimbo madogo madogo manne.Baada ya kutoelewana hapo ugomvi ulianza lakini ulichagizwa zaidi baada ya Katumbi kuona Rais Kabila hana nia ya kuachia madaraka na akatoa kauli ya kumtaka atoke madarakani muda unapokwisha November mwaka huu.
Kukazia zaidi Katumbi alitangaza nia yake ya kugombea urais na ndiop[o hapo vita yake na Rais Kabila vilipamba moto.
 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment