Mjeshi Ashinda Shindano La Juu La Urembo Marekani “Miss USA”


 
Katika hali isiyotarajiwa tena kwa mara ya kwanza mwanajeshi mrembo Bi. Deshauna Barber mwenye umri wa miaka 26 ameibuka mshindi katika shindano la kumtafuta mrembo wa Marekani lililofanyika hapo jana.Bi Barber afisa wa jeshi kutoka jimbo la Columbia sio tu ni mrembo bali jibu lake alilolitoa wakati wa kipindi cha maswali na majibu ndilo lililowapagawisha zaidi majaji.
 
Akiulizwa analiongeleaje suala la wanawake kuwa katika jeshi alisema “Kama mwanamke hapa Marekani nadhani tupo imara sawa na wanaume.Nikiwa kama kiongozi wa kombania yangu nina nguvu, ninajitoa na niko imara. Jinsia haitufungi sana hapa Marekani tuko sawa kabisa na wanaume” alimalizia.


Akiwa kama mshindi wa shindano hilo lililofanyika T-Mobile Arena nje kidogo mwa jiji la Las Vegas Barber atashiriki shindano la dunia.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment