Kikwete Amfanyia “Ukuda’’ Magufuli,Ni Kuhusu Nchi Kujitegemea




 
Wakati Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli akisisitiza kuwa nchi za kiafrika ni lazima sasa zijipange ili zijitegemee Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete jana amesema hilo haliwezekani na kuwa ni lazima nchi za kiafrika zijipange na kujiwekea utaratibu wa namna ya kupokea misaada kutoka nchi za ulaya kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.
Kikwete aliekuwa akifungua mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya umoja wa Mataifa yanayohusu “Maendeleo Endelevu kwa mwaka 20130” amesema nchi za ulaya kutupa sisi nchi za kiafrika misaada ni jukumu lao la kihistoria maana walitutawala na kuendeleza nchi zao kwa kutumia rasilimali zetu hivyo wanao wajibu wa kuturudishia kwa njia za kimisaada.
Swali ambalo wachambuzi na wataalamu wanajiuliza ni kama kweli misaada hii inatukomboa kama bara la Afrika ama inazidi kutupumbaza na kutubakisha nyuma.Mwandishi wa vitabu na msomi aliebobea Profesa Dambisa Moyo katika kitabu chake cha Dead Aid alieleza kuwa misaada haikuwahi,haiwahi na haitakaa iwahi kutusaidia sisi kama bara la Afrika kuendelea.
Je,Kikwete anamfanyia ukuda Magufuli?
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment