Virus Vya Zika Sasa Vyawezekana Kuwepo Tanzania


Shirika La Afya Duniani WHO limesema virusi vya Zika sasa vimeingia Afrika  kwa kuanzia na Cape Verde na kuwa kuna uwezekano wa kusambaa nchi yoyote kama hatua stahiki hazitachukuliwa.Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa shirika hilo kwa kanda ya Afrika Dkt.Matshidisco Moeti alisema “Taarifa hii itazisaidia nchi za Afrika kujitathmini na kuchukua tahadhari na kuongeza utayari wao wa kupambana navyo”
Alisema nchi za kiafrika sasa ziongeze umakini kwa mama wajawazito na kuwahimiza watu kujikinga na mbu na maambukizi kwa njia ya ngono.Lakini akasisitiza kuwa haungi mkono njia zozote za kupambana na virusi hivi kwa kuzuia watu kusafiri.

Mpaka sasa watu zaidi ya 7,000 wameripotiwa kuwa na virusi hivi huko Cape verde,na kati ya hao tayari wajawazito 180 wameshaathirika navyo.Watoto watatu tayari washazaliwa wakiwa wameharibka ubongo.
Mpaka pale virusi hivi vilivyothibitishwa na wanasayansi nchini Senegal ilikuwa bado haijajulikana kama ni virusi jamii ya Afrika ama ile ya Asia iliyoikumba Brazil.Lakini sasa imethibitishwa virusi hivi ni jamii ileile iliyoikumba Brazil vyenye asili ya bara la Asia na kusababisha matatizo makubwa ya ubongo kwa watoto waliozaliwa.

Mtafiti wa Kiingereza alisema kuwa virusi vya Zika vimekuwapo Afrika kwa zaidi ya miaka 50 hivyo jamii nyingi inaweza kuwa tayari imeshajitengenezea kinga tofauti na nchi za Amerika ya kusini ambapo ndio kwa mara ya kwanza na ndio maana wakiumwa na mbu tu wanaathirika.

Fahamu:
Virusi vya Zika kwa mara ya Kwanza viligundulika Afrika mwaka 1947 lakini vikiwa havina athari yoyote na ubongo tofauti na sasa.

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment