Kushiriki Mdahalo Na Sanders Kwa Sasa Ni Kupoteza Muda – Clinton


Mgombea urais anayeonekana kuongoza katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amekataa kushiriki mdahalo dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders.
Maafisa wake wa kampeni wamesema badala yake, Bi Clinton ameonelea ni heri kukabiliana na mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump kuliko kupoteza muda huo kufanya mdahalo na Bw. Sanders.
Bi Clinton alikuwa awali amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.
Bw Sanders, Seneta wa Vermont, amesema hajashangazwa na uamuzi huo wa mpinzani wake.
Wapo wachambuzi wanaodai labda uamuzi huo wa Bi. Hillary ni kutotaka kuharibiwa na Bw Sanders anaeonekana kuwa mwiba mkali katika midahalo ama ni kwa sababu ameona anaongoza hivyo ni afadhali ajipange kukabiliana na mgombea wa Republican Bw Trump anaeonekana ndie atakayepitishwa na chama chake katika kinyang’anyiro hicho.
Na katika hatua inayoonesha viongozi wa Democratic hawataki kumtenga Bw Sanders na wafuasi wake, wametangaza kwamba mgombea huyo ataruhusiwa kuteua theluthi moja ya kamati ya kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwezi Julai.
Mkutano huo hutumiwa kuidhinisha mgombea urais wa chama cha Democratic.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.
 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment