Bosi wa TP Mazembe Moise Katumbi Sasa Rasmi Urais DRC. Kupambana na Joseph Kabila

Mfanya biashara tajiri na mmiliki wa timu kali ya mpira wa miguu ya TP Mazembe MOISE Katumbi jana alitangaza rasmi kuwania kiti cha urais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Katanga na mmiliki wa migodi kadhaa ya dhahabu ameweka wazi nia yake hiyo huku akimuonya Rais Joseph Kabila kutoingiza nia ovu ya kutaka kugombea tena madaraka kwa kuichakachua katiba ambayo kwa sasa haimruhusu kufanya hivyo.

Kuna tetesi kuwa Rais Kabila yupo kwenye mpango kabambe wa kutaka katiba ibadilishwe ili aweze kugombea tena Urais jambo ambalo Katumbi amesema linaweza kusababisha machafuko makubwa. Katumbi anaetarajiwa kuendesha kampeni nzito kutokana na uwezo wake wa kifedha tayari amaeshaanza kuwa tishio na kwa chama kinachotawala sasa maana tayari vyama kadhaa vya upinzani vimeshatangaza kumuunga mkono. Ametangaza kugombea nafasi hiyo kama mgombea binafsi.

Katumbi amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka hu 2016 amekuwa akitoa kauli zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo mtaka kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.

Licha ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu kwake 2015.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wa uongozi wake.


Wachunguzi wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment